Mhe. Balozi Issa Suleiman Nassor akikagua baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na kiwanda cha kusindika samaki cha Kampuni ya “Summer Moon” kilichopo katika eneo la Borge Arab, Alexandria tarehe 16 Oktoba, 2018. Mhe. Balozi Nassor aliuomba uongozi wa Kampuni hiyo kuangalia uwezekano wa kutembelea Tanzania kwa ajili ya kuangalia fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji hususan katika sekta ya uvuvi na viwanda vya usindikaji samaki.