Mhe. Exaud Silaoneka kigahe, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Tanzania tarehe 27/01/2025 amelifungua kongamano la siku moja la kuhamasisha uwekezaji nchini Tanzania lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Alexandria Chamber of Commerce.

Mhe. Exaud Kigahe ameongoza ujumbe wa Tanzania uliowasili nchini Misri kuhamasisha uwekezaji nchini Tanzania ambapo aliwashajihisha wafanyabiashara waliopo Alexandria kuwekeza mitaji yao Tanzania kutokana na mazingira mazuri ya uwekezaji, eneo la kijiografia la Tanzania ni lango la kibiashara kuingia Ukanda wa Afrika Mashariki na nchi za Kusini mwa Bara la Afrika (SADC).

Aidha, Tanzania inayo rasilimali nyingi katika sekta ya kilimo, madini na rasilimali maji, kupitia mito, maziwa na bahari ya Hindi.

Vile vile, utulivu wa kisiasa uliopo, vivutio vingi vya misamaha ya kodi na uwepo wa kituo cha uwekezaji cha TIC ni miongoni mwa sababu muhimu kuwekeza nchini Tanzania.

Nae Mhe. Meja Generali Richard Mutayoba Makanzo, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri alitumia fursa kuwakaribisha Wafanyabiashara wa Misri kupata taarifa mbali mbali za uwekezaji ili kuimarisha uhusiano zaidi baina ya Misri na Tanzania kupitia Wataalamu waliohudhuria kongamano hilo.