Mheshimiwa Maj. Gen. Richard Mutayoba Makanzo, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri, tarehe 27 Machi, 2025 amekutana na Diaspora waliopo nchini Misri katika hoteli ya Pyramisa iliopo Dokki, Cairo.
Aliwasisitiza Diaspora hao kuwa Mabalozi wazuri kwa nchi yao, kudumisha upendo, undugu, umoja na mshikamano ili kutunza jina zuri, heshima na sifa ya nchi.
Aidha, aliwataka kusaidia juhudi za Ubalozi kutafuta fursa za uwekezaji katika sekta ya Afya, kilimo, viwanda, uvuvi wa Buluu na miundombinu.
Nae Mlezi wa Diaspora Ndugu Rashid Haroun alisisitiza umuhimu wa kufuata mila, desturi, sheria na kanuni za Misri. Sambamba na hayo, aliwasihi kuzingatia malengo yao kwa kujiwekea hakiba, wale wanafunzi kuzingatia masomo yao ili wamalize kwa mafanikio.
Nae Bi. Zaituni Abdallah Nassor, Mwenyekiti wa Umoja wa Watanzania waishio Misri alisisitiza umoja, upendo na mshikamano miongoni mwa Diaspora na alitoa wito wa kuwataka waliokuwa hawajajiunga na umoja huo Kufanya haraka kujiunga.
Hafla hiyo iliwahusisha Diaspora, Maafisa wa Jeshi waliopo masomoni nchini Misri, Maafisa wa Ubalozi na familia zao pamoja na Wanafunzi wanaosoma vyuo mbalimbali vilivyopo Cairo.