Tarehe 28 Machi, 2025 Mhe. Meja Jenerali Richard Mutayoba Makanzo, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri ameungana na Watanzania wengine kuipokea Timu ya Simba S.C. ambayo  imeweka kambi ya muda mfupi katika mji wa Ismailiya nje kidogo ya Mji wa Cairo.

Mapokezi hayo yameambatana na ngoma  iliyoandaliwa na wapenzi wa Simba S.C. waliopo Cairo ambao kwa kushirikiana na Ubalozi watafurika katika uwanja wa Suez Canal Stadium tarehe 2 Aprili, 2025 watakapomenyana vikali na Al-Masry ya Misri katika hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAFCC).

Mchezo huo pia utashuhudiwa na Mashabiki wa Simba  ambao ni Watanzania  Walioko katika mji wa Alexandria chini ya uratibu wa Ubalozi.