Mhe. Meja Jenerali Richard Mutayoba Makanzo, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri akiwa na ujumbe wa Tanzania uliofika nchini Misri kuhamasisha uwekezaji nchini Tanzania unaoongozwa na Mhe. Exaud Silaoneka Kigahe, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Tanzania, tarehe 25 Januari, 2025 Wametembelea mradi mkubwa wa ujenzi wa Nyumba za makazi na Biashara ILMONTE GALALA uliopo Sokhna nchini Misri ambapo Villa zenye vyumba elfu 10 zinatarajiwa kujengwa ifikapo mwaka 2033.
Mradi huu wa aina yake unajengwa kwenye eneo la milima na unajengwa hatua baada ya hatua baada ya kukata milima na unatarajiwa kugharimu hadi paundi za Misri Bilioni 7 hadi kukamilika kwake.
Miradi kama hiyo pia ipo Dubai na Saudi Arabia. Mhe. Exaud Kigahe alifurahishwa na ujenzi wa mradi huo mkubwa na amewakaribisha wawekezaji hao nchini Tanzania kujenga nyumba za makazi, hoteli pamoja na fursa nyingi zilizopo katika Kilimo.
Wawekezaji hao wameahidi kufika Tanzania na kabla ya ujumbe huo kuondoka nchini Misri, wameomba kufanya mazungumzo ili kupanga tarehe za kutembelea nchini Tanzania.