Siku ya tarehe 20 Machi, 2023 Maafisa wa Ubalozi, ndg. Makame Iddi, Mkuu wa Utawala na ndg. Rashid Haroun, Mwambata Siasa, Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kampuni ya AllMed Middle East Company ya Misri baada ya kutembelea Kiwanda cha Kampuni hiyo kinachotengeneza mashine za dialysis za kutibu maradhi ya Figo pamoja na dawa zake.
Kampuni hiyo tayari imeshafungua tawi la kampuni hiyo nchini Tanzania eneo la Masaki - Dar es Salaam na ghala la kuhifadhia bidhaa zao likiwepo Kariakoo - Dar es Salaam.