Mhe. Innocent Bashungwa (MB), Waziri wa Viwanda na Biashara wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akifanya mazungumzo na Mhandisi Ahmed El Sewedy, Mwenyekiti wa Kampuni ya El Sewedy Electric ya Misri tarehe 23 Novemba, 2019. Mhe. Waziri Bashungwa alishawishi uongozi wa El Sewedy Electric kuangalia uwezekano wa kuwekeza nchini Tanzania katika sekta ya viwanda vya kutengeneza vifaa vya umeme.