Mhe.Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akizungumza kwenye Mkutano wa Waandishi wa Habari baada ya kikao cha pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Mhe. Sameh Shoukry tarehe 09/06/2022. Viongozi hao walisisitiza haja ya kuimarisha mahusiano ya kihistoria kati ya nchi zao mbili pamoja na kuendeleza zaidi mashirikiano katika sekta mbali mbali ikiwa ni pamoja na elimu, afya, nishati, ulinzi na usalama, kilimo cha kisasa, uhifadhi wa mazingira na matumizi bora ya teknolojia katika uboreshaji wa maendeleo katika sekta mbali mbali. 

Pia, kuendeleza vikao vya Kamati ya Pamoja ya Kudumu (JPC), ushiriki wa Tanzania katika Mkutano wa 27 kuhusu mabadiliko ya Tabia nchi (COP27), uungaji mkono wa Tanzania kwa Misri katika ufanikishaji wa mkutano wa 27 wa Mabadiliko ya Tabia nchi.