Leo tarehe 04/08/2022 Mhe. Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri Mhe. Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa ofisini kwake alitembelewa na Walimu na Wanafunzi wa Shule ya msingi ya Feza – Kawe waliopo nchini Misri kwa ziara ya kimasomo. 

Naye Mhe. Balozi aliwakaribisha ubalozini na aliwapa somo fupi juu ya historia ya kuanzishwa kwa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini  Misri pamoja na Mabalozi waliohudumia Ubalozi huo na mwisho kabisa aliwapa zawadi maalum kila mmoja wao ikiwa ni kumbukumbu kutoka Ubalozini