Tarehe 05 Aprili, 2019, Balozi Issa S. Nassor akiwa na Waziri wa Elimu ya Juu wa Misri wakishuhudia uwekaji saini wa Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar na Chuo Kikuu cha Alexandria jijini Cairo nchini Misri. Uwekaji saini huo umefanywa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar, Prof. Idris Rai na Rais wa Chuo Kikuu cha Alexandria, Prof. Essam El Kordy.
