Tarehe 05/2/2024 Mhe. Mej. Gen. Richard Mutayoba Makanzo, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri alifanya ziara kuitembelea Taasisi ya Arab Organization for Industrialization (AOI) katika mji wa Nasser City, Cairo.

Taasisi hiyo ni mkusanyiko wa Makampuni 14 ambayo 7 kati ya hayo yapo chini ya Jeshi la Misri na mengine 7 yaliyobakia yanamilikiwa na watu binafsi.

Taasisi ya AOI inajihusisha na uzalishaji na uunganishaji wa Magari ya Kijeshi, Polisi, zimamoto, magari ya kusafirishia fedha, magari yenye ofisi zinazotembea (mobile offices), vifaa vya kijeshi kama vile Ndege Nyuki (drones), vifaa vya kilimo pamoja na vifaa vya matumizi ya nyumbani kama vile majokofu, Televisheni, vipoza hewa, mashine za kufulia na kadhalika.
Lengo la ziara hiyo ni kimarisha uhusiano na Taasisi ya 'AOI' na kuona utendaji wa Taasisi hiyo na vifaa vinavyozalishwa na Makampuni yaliopo chini ya Taasisi hiyo.

Viongozi wa Taasisi ya Arab Organization for Industrialization wanatarajia kufanya ziara nchini Tanzania kwa ajili ya kukutana na viongozi wa Wizara, Taasisi na Makampuni mbali mbali ya Tanzania kujadili namna bora ya kushirikiana kibiashara, kubadikishana bidhaa na kadhalika.