Mej. Jen. Richard Mutayoba Makanzo, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri ameitembelea kampuni ya Multipharm ya Assiut nchini Misri ikiwa ni juhudi za kutafuta wawekezaji kwa ajili ya kuingiza mitaji nchini Tanzania kutoka nje ya nchi.

Kampuni hiyo inakusudia kuwekeza kwa kujenga kiwanda cha dawa za virutubisho vya wanyama wa kufuga kama kuku, ng'ombe na kadhalika, mbolea pamoja na vyakula vya wanyama.

Kampuni inakusudia kushiriki maonyesho ya 48 ya  Kimataifa ya Biashara (sabasaba) kuangalia soko bidhaa hizo nchini Tanzania.

Ziara hiyo imefanyika tarehe 09 Juni, 2024 lengo ni kuangalia uwezo wa Kampuni pamoja na Ofisi za Kampuni ili kutambulishwa rasmi katika Mamlaka za Uwekezaji na Biashara nchini Tanzania.

Mhe. Balozi aliwakaribisha wawekezaji hao kwa kuwa Tanzania ni Nchi ya amani na imeweka mazingira mazuri kwa wawekezaji fursa ambayo itawezesha kupata soko kubwa la Afrika Mashariki na soko la nchi za Kusini mwa Africa (SADC).