Siku ya tarehe 03/04/2024 Mhe. Brigedia Jen. Ismail Shajack Ismail (Kaimu Balozi) akiambatana na Maafisa wa Ubalozi walifika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Cairo kwa ajili ya kupokea ujumbe na timu ya simba iliyofika nchini Misri kwa ajili ya kukamilisha mechi ya hatua ya Robo Fainali ya CAF Champions League kati yake na timu ya Al Ahly itakayochezwa katika uwanja wa Cairo Stadium siku ya Ijumaa tarehe 05/04/2024.