Leo tarehe 06-04-2024 Brig. Jen. Ismail Shajack Ismail pamoja na Maafisa Ubalozi  walifika katika Hoteli waliyofikia Timu ya Simba Sc na kuambatana nao hadi uwanja wa ndege wa kimataifa wa Cairo kwa ajili ya kuagana. Ikumbukwe kuwa timu ya samba ilikuwa Misri kwa ajili ya kucheza mechi ya marudiano kati yake na timu ya Al Ahly.

Brig. Jen. Ismail Shajack Ismail akimuakilisha Mhe. Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri Mej. Jen. Richard M. Makanzo aliupongeza Uongozi na timu ya Simba Sc kwa juhudi zinazofanywa na kusisitiza umoja ndani ya timu ikiwa sambamba na kutokata tamaa katika matokeo ya michezo inapokuwa ni hasi.

Mwisho aliwatakia safari njema na matokeo mazuri zaidi katika mashindano ya Kitaifa na ya Kimataifa kwa msimu ujao.
wauaga