Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - (Uwekezaji) Mhe. Geoffrey I. Mwambe na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Dkt. Maduhu. I. Kazi  wameshiriki katika kongamano la Taasisi za Uwekezaji Afrika lililofanyika Sharm El Sheikh nchini Misri. Kongamano hilo linaongozwa na Mhe. Dkt. Mostafa Madbouly, Waziri Mkuu wa Misri kuanzia tarehe 11 hadi 14 June, 2021. Mhe. Waziri wa Uwekezaji Mwambe na Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Dkt Maduhu wamefanya mikutano mingine na wawekezaji mbalimbali waliowekeza nchini Tanzania na ambao walionyesha nia ya kuwekeza nchi kutokana na sera nzuri na mazingira ya uwekezaji yaliyopo nchini.