Timu ya Taifa Stars ya Tanzania imeshinda goli 1 kwa 0 dhidi ya Timu ya Taifa ya Uganda katika mashindano ya kufuzu kuingia mashindano ya Klabu Bingwa Afrika (AFCON2023).

Mechi hiyo ilichezwa katika uwanja wa Suez Canal Authority Stadium, uliopo mkoa wa Ismailiya, nchini Misri tarehe 24 Machi, 2023 saa 10:00 jioni saa za Misri, sawa na saa 11:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Ushindi huo mnono unaipatia Taifa Stars pointi 4 muhimu kutokana na Mashirikiano mazuri ya Ubalozi wa Tanzania Misri, TFF, na Wizara ya Michezo ambapo Mhe. Hamis Mohamed Mwinjuma, Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo alihudhuria pambano hilo chini ya hamasa kubwa ya Watanzania wanaoishi Misri wakiongozwa na Mhe. Emmanuel John Nchimbi, Balozi wa Tanzania nchini Misri.