Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Cairo, Misri ukiongozwa na Balozi Dr Emmanuel Nchimbi uliandaa sherehe za miaka 59 ya Muungano wa Tanzania tarehe 26 April 2023, sherehe hizo ziliandaliwa kwa ushirikiano na Benki ya CRDB. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilizaliwa tarehe 26 Aprili, 1964 baada ya uamuzi maridhawa wa wananchi wa Tanganyika wakiongozwa na Hayati Rais Julius Nyerere na wanannchi wa zanzibar wakiongozwa na Hayati Rais Abeid Karume na kupelekea kuzaliwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sherehe za maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano zilipambwa na tenzi, ngoma za utamaduni kutoka kikundi cha Watanzania wanaoishi nchini Misri cha Victoria Cultural Group, wasilisho muhimu kuhusu huduma za CRDB, kukata keki maalum, wasilisho la mada maalum ya miaka 59 ya Muungano kutoka kwa Diaspora, pamoja na nyimbo maalum za kumpongeza Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, kwa kuweszesha kuifungua Tanzania Kiuchumi, kisiasa, Kidiplomasia n.k.
Aidha, kwenye sherehe hizo zilihudhuriwa na Mabalozi mbali mbali kutoka nchi rafikia za Msumbiji, Namibia, Zambia, Mauritius, Angola, Namibia na wawakilishi kutoka Ubalozi wa Kenya na Malawi mwakilishi kutoka Egypt- African Center for Strategic Studies, ALAMEDA Groups of Hospitals, Mwakilishi kutoka Egyptian-African Business Association (EABA), Wawakilishi kutoka Benki ya CRDB, watumishi wa Ubalozi, Wanajeshi wanaosoma nchini Misri, watanzania mbali mbali wanaoishi na kusoma Vyuo vya Elimu ya Juu nchini Misri.