Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Mhe. Sameh Shoukry amemshukuru Balozi wa Tanzania nchini Misri anaemaliza muda wake Dr. Emmanuel Nchimbi kwa kazi kubwa aliyofanya ya kuimarisha uhusiano wa Tanzania na Misri. Amesema Tanzania kwa sasa ni moja nchi rafiki wa kuaminiwa sana na Misri. 

Waziri Shoukry amesema  alipokuwa akimuaga Rasmi Balozi Nchimbi  ambaye amemaliza Muda wake wa Ubalozi Nchini Misri.

Kwa Upande wake Balozi Nchimbi amemshukuru Waziri Shoukry na Serikali ya Misri kwa ushirikiano mkubwa waliompatia wakati akitimiza majukumu yake na ameomba wampe ushirikiano Balozi Mpya wa Tanzania Nchini Misri.