Mhe, Meja Jenerali Anselm S. Bahati, Balozi wa Tanzania nchini Misri atembelewa na vijana wa Scout-Tanzania wakiongozwa na Bw. Faustin Magige Kamishna Msaidizi wa Scout-Tanzania, tarehe 20 Desemba, 2019. Mhe. Balozi Bahati alitumia nafasi hiyo kuwapa mafunzo vijana hao wa Scout-Tanzania na viongozi wao juu ya shughuli za ubalozi. 

Baada ya mafunzo hayo, Mhe. Balozi Meja Jenerali Bahati aliwakaribisha vijana hao pamoja na viongozi wao takriban 70 kwenye chakula cha mchana kilichojumuisha pia viongozi wa Jumuiya ya Watanzania waishio nchini Misri na viongozi wa Wanafunzi wa Tanzania wanaosoma katika vyuo mbalimbali nchini Misri. Mhe. Meja Jenerali Anselm S. Bahati aliwasisitiza vijana hao wa Scout pamoja na viongozi wao kuendelea kuwa Wazalendo kwa nchi yao Tanzania na Serikali kwa ujumla.