Siku ya tarehe 23/07/2022 Balozi wa Tanzania nchini Misri Mhe. Emmanuel John Nchimbi akiwa na mchezaji wa Simba Pape Osmane Sakho, aliyebeba tuzo ya kiatu cha dhahabu cha mfungaji wa bao bora la Africa 2022 na Barbara Gonzalez Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Cairo Misri.
Wakati huo huo, Maafisa wa Ubalozi wa Tanzani Misri kwa pamoja walifurahia kiatu cha dhahabu na mchezaji wa Simba Sport Club, Pape Osmane Sakho aliyeshinda goli bora la Africa 2022 - CAF 2022 (CAFAwards2022) na kumtakia mafanikio zaidi katika hatua zake zijazo.


