Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri Mhe. Sameh Shoukry aliongea kwa njia ya simu siku ya Jumapili 05 Juni, 2022 na Mhe. Liberata Mulamula, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  na kujadiliana kuhusu masuala  tofauti ya mahusiano na yenye masilahi kwa nchi mbili. 

Aidha, katika muktadha wa mazungungumzo yao, Mawaziri hao wawili walikubaliana kuendelea na vikao vya Kamati ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya nchi hizo mbili ili kuimarisha ushirikiano wa pande mbili katika nyanja zote.

Waziri wa Mambo ya Nje alisisitiza nia ya Misri kuendelea kutoa msaada kwa Tanzania katika nyanja mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuunga mkono juhudi mbalimbali za maendeleo nchini Tanzania.