Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally aliwasili nchini Misri kutokea Tanzania tarehe 05 Juni, 2022 na ujumbe wake wa watu watatu kwa kuitikia mwaliko wa kuhudhuria  Mkutano ulioandaliwa na Serikali ya Jamhuri ya Kiarabu ya Misri chini ya Ofisi ya Mhe. Mufti wa Misri. 

Aidha, siku ya tarehe 06 Juni, 2022 Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania alipata nafasi ya kumtembelea Mwenyeji wake Mhe. Balozi wa Tanzania Dkt. Emmanuel J. Nchimbi nyumbani kwake na kupata karamu ya pamoja iliyondaliwa na Mhe Balozi.

Pia katika yaliyojiri Mhe. Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania alimuombea Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan  pamoja na Taifa la Tanzania  kwa ujumla Baraka, utulivu na mafanikio mema.