Rais Abdel Fattah El-Sisi alitoa salamu zake za rambirambi na mkono wa pole kwa Wananchi na Serikali ya Jamhuri ya Tanzania juu ya kifo cha Mheshimiwa Rais, John Magufuli, Rais wa Tanzania, ambaye alifariki baada ya kazi kubwa aliyoifanya ya kuwahudumikia wananchi na mchango wake mkubwa katika kuleta maendeleo kwa watu wake, nchi yake na Bara la Afrika.
Kutokana na uhusiano madhubuti wa kindugu uliopo kati ya Misri na Tanzania, Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Serikali na watu wake, wathibitisha kuungana na kushikamana pamoja na ndugu zao Watanzania katika msiba huu mkubwa wakimwomba Mwenyezi Mungu amrehemu, ambariki na amsamehe kwa rehema zake na kuwapa subira, faraja na uvumilivu kwa wapendwa wote.
https://www.presidency.eg/ar

