Mhe. Job Y. Ndugai (Mb), Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akitembelea shamba la Lamar lililopo katika Mkoa wa Alexandria – Misri tarehe 20 Juni, 2019. Akiwa kwenye shamba hilo Mhe. Ndugai alipata maelezo ya namna shamba hilo linavyoendeshwa kwa mafanikio makubwa. Shamba hilo la Lamar linajishughulisha na kilimo cha mazao mbalimbali yakiwemo mahindi, zabibu, makomamanga, na mazao mengine pamoja na kushughulika na ufugaji wa ng`ombe wa maziwa. Kampuni ya Lamar pia ina viwanda vya usindikaji na utengenezani wa maziwa na juisi ya kila aina ya matunda.
