Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa na Mhe. Sahar Nasr, Waziri wa Uwekezaji na Ushirikiano wa Kimataifa wakati wa Mkutano na Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Misri tarehe 08 Julai, 2019. Mhe. Waziri Mkuu alieleza fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji zilizopo nchini Tanzania na kusikiliza changamoto zinazowakabili Wafanyabiashara hao katika uwekezaji wao nchini Tanzania.
