Tarehe 20-04-2022 Mjumbe maalum wa Rais Abdel fatah Alsis, Bw. Ahmed Reda amemtembelea balozi wa Tanzania Nchini Misri Dr Emmanuel Nchimbi ili kufikisha Salaam kwa Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan.
Baada ya kuupokea ujumbe huo Balozi Nchimbi alimshukuru Rais Alsis na alimhakikishia mjumbe huyo kuwa  ujumbe huo utafikishwa kwa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan.