Mhe. Balozi Meja Jeneral Anselm Bahati, Balozi wa Tanzania nchini Misri akizungumza na viongozi wa Jumuiya za Watanzania waishio nchini Misri na Jumuiya ya wanafunzi wa Tanzania wanaosoma nchini Misri tarehe 27 Desemba, 2019. Katika mazungumzo hayo, Mhe. Balozi Bahati aliwasisitiza viongozi hao kudumisha umoja, msikamano ili kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Ubalozi na Jumuiya hizo. Aidha, Mhe. Balozi Bahati aliwataka viongozi hao kufuata sheria za nchi wanayoishi na kuepuka migogoro isiyo ya lazima.

  • Picha ya pamoja kati ya Mhe. Balozi Bahati na baadhi ya Watanzania walipokutana kwa ajili ya kujitambulisha na kupata chakula cha jioni tarehe 27 Desemba, 2019.Picha ya pamoja kati ya Mhe. Balozi Bahati na baadhi ya Watanzania walipokutana kwa ajili ya kujitambulisha na kupata chakula cha jioni tarehe 27 Desemba, 2019.
  • Baadhi ya Watanzania wakifiatilia kwa karibu hotuba ya Mhe. Balozi Bahati wakati akizungumza na Watanzania waishio nchini Misri tarehe 27 Desemba, 2019.Baadhi ya Watanzania wakifiatilia kwa karibu hotuba ya Mhe. Balozi Bahati wakati akizungumza na Watanzania waishio nchini Misri tarehe 27 Desemba, 2019.