Picha ya pamoja kati ya Mhe. Meja Jenerali Issa Suleiman Nassor, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri na Uongozi wa Chuo cha Mubarak baada ya kutembelea Chuo cha Ufundi Stadi cha Mubarak Kilichopo katika mji mdogo wa Borge Arab, Alexandria tarehe 16 Oktoba, 2018. Mhe. Balozi Nassor alielezwa namna vijana wanavyoandaliwa katika Ufundi Stadi ili waweze kujitegemea na wengine kuajiriwa katika maeneo mbalimbali ya Uzalishaji ikiwemo viwanda. Vijana hao wanapata mafunzo ya kushona nguo, umeme, elektroniki, mechanical na fani nyenginezo.