Tarehe 31 Januari, 2024 Mhe. Mej. Gen. Richard Mutayoba Makanzo, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri akiwa na Wakaguzi kutoka Tanzania Medical and Drug Authority (TMDA) ameshiriki ukaguzi wa kiwanda cha Global Pharmaceutical Group ( GPI) kilichopo Mji wa 6th October City, nje kidogo ya Mji wa Cairo. 

Kiwanda hicho kinaongozwa na Dr. Peter Makram Mehany, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mwendeshaji kilianzishwa 2009 na kuanza uzalishaji mwaka 2010 kwa uzalishaji wa dawa za sindano pekee zaidi ya bidhaa 150. 

Kiwanda hicho ni miongoni mwa viwanda 10 bora nchini Misri kwa utengenezaji dawa kwa matumizi ya Binaadam nchini Misri.

 Ukaguzi huo unafanyika ikiwa ni hitajio la kisheria kabla dawa za kiwanda hicho kuingia katika soko la Tanzania.