Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Cairo, Misri uliandaa hafla maalum tarehe 29/04/2022 kwa ajili ya kumtambulisha Balozi mpya Mhe. Emmanuel John Nchimbi kwa Watanzania wanaoishi Cairo,  Wanafunzi na Wanajeshi waliopo Cairo kwa mafunzo katika vyuo mbali ambapo walijumuika pamoja katika futari ya pamoja iliyoandaliwa na Mhe. Balozi nyumbani kwake. Katika Hafla hiyo, Mhe.Balozi aliwahakikishia Watanzania na wanafunzi wote kwamba Ubalozi utaendelea kushirikiana nao na kufanyakazi nao ili kuliletea Taifa la Tanzania Maendeleo ya haraka. Pia, aliwasihi Watanzania kuzingatia sheria na taratibu za nchi ili Ubalozi upate nguvu ya kuwatumikia vizuri. Pia, aliwakumbusha kuwa Ubalozi upo kwa ajili ya kulinda maslahi ya nchi, kuimarisha mahusiano na mashirikiano pamoja na kuwatumikia Watanzania wanaoishi Misri, hivyo tuishi kwa kufuata, sheria, maadili na taratibu za nchi na walatusijisahau kwamba tuko ugenini.