Tarehe 21/07/2022, Mhe. Balozi alikutana viongozi wa Mamlaka ya Huduma za Afya nchini Misri kupitia Idara ya uhamasishaji wa huduma za Afya kupitia utalii(medical tourism department). Mamlaka hiyo inakusudia kuanzisha mashirikiano na Serikali ya Tanzania kuimarisha utoaji wa huduma za afya, kujenga uwezo wa madaktari bingwa, kubadilishana uzoefu na ujuzi, kuandaa kambi tiba pamoja na kutoa fursa kwa wagonjwa kutoka Tanzania kutibiwa nchini Misri.

