Siku ya tarehe 08 Januari, 2023, Mhe. Balozi Mej. Gen. Richard Mutayoba Makanzo, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri ameambatana na Maafisa wa Ubalozi kuitembelea Kampuni ya Rowad Modern Engineering ya Misri kwenye Makao Makuu huko New Cairo.

Alipata nafasi ya kukagua shughuli za kiutawala katika idara mbali mbali, pia alitembelea miradi inayotekelezwa na Kampuni hiyo katika mji mpya wa kiutawala ikiwa ni pamoja na ujenzi wa viwanja vya kisasa vya michezo mbalimbali katika Sport City.

Pia, alitembelea chuo kikuu cha Knowledge Hub University, kilichojengwa na Kampuni hiyo ndani ya miezi 10 hatua ya mwanzo.

Pia alitembelea mradi wa nyumba za makazi na sehemu za biashara wa Mivida Complex, katika mji wa New Cairo  zinazojengwa na kampuni hiyo kwa lengo la makazi na sehemu za Biashara.

Kampuni hiyo inatarajia kuingia soko la Tanzania kutekeleza miradi ya ujenzi wa viwanja vya michezo vya kisasa nchini Tanzania ikiwa ni juhudi za kutafuta wawekezaji kusaidia utekelezaji wa diplomasia ya uchumi na viwanda nchini Tanzania.