Mhe. Maj. Gen. Richard Mutayoba Makanzo, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri tarehe 22/07/2024 ameitembelea timu ya Simba Sports Club katika mji wa Ismailiya nje kidogo ya Cairo ambapo alishuhudia mchezo mzuri wa mechi ya kirafiki baina Simba na Canal Sporting Club ya Misri.

Balozi Makanzo ameipongeza timu ya Simba kwa kusajili vijana wazuri pamoja na kuimarisha mahusiano mazuri yaliyopo baina ya Misri na Tanzania kupitia sekta ya michezo.

Katika mchezo huo Simba ilitoka kifua mbele kwa kuifunga Canal bao 3 kwa sufuri.

Aidha, kabla ya mchezo huo, Mhe. Maj Gen. Richard Mutayoba Makanzo Alizungumza na uongozi wa timu ya Canal Sporting Club ambapo aliwakaribisha Tanzania kujionea vivutio mbali mbali vya utalii pamoja na kuwekeza Tanzania kutokana na wingi wa Rasilimali zilizopo ikiwa ni pamoja na  Madini ya dhahabu, Almasi, Tanzanite, Mlima Kilimanjaro, fukwe za Zanzibar, wanyama wakubwa Duniani kama vile Simba, Chui, Tembo, Kifaru na kadhalika ili kuendeleza mahusiano hayo na kunufaika na fursa za kiuchumi.