Tarehe 29 Januari, 2024 Mhe. Mej. Gen. Richard Mutayoba Makanzo, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri ameambatana na wakaguzi wa viwanda vya Madawa kutoka Tanzania Medical Drugs Authority (TMDA) katika ukaguzi wa kiwanda cha kutengeneza dawa cha Utopia Pharmaceuticals kinachomilikiwa na Dkt. Saied Kamel huko 10th Ramadhan City, Barabara ya Ismailiya, nje kidogo ya Mji wa Cairo.
 Wakaguzi hao watakagua viwanda 4 vya utengenezaji dawa za binaadam ikiwa ni zoezi maalum la kawaida kwa ajili ya kuangalia udhibiti wa kupunguza maambukizi au kuingia vitu visivyohitajika katika mchakato mzima wa utengenezaji wa dawa kwa matumizi ya binaadamu.
Viwanda hivyo vimeomba kuingiza katika soko la Tanzania dawa zinazotengenezwa nchini Misri. Hivyo, ukaguzi unafanyika ikiwa ni hitajio la kisheria kujiridhisha usalama, ubora, na mchakato mzima wa utengenezaji wa dawa hizo kabla ya kuingizwa katika soko la Tanzania. 
Ukaguzi huo unafanywa na Bw. Adam M. Fimbo, Bw. Magana Bundala Maganga na Bw. Frederick Samson Luyangi kuanzia tarehe 28 Januari, 2024 hadi tarehe 09 Februari, 2024 watakapoondoka