Mhe. Job Y. Ndugai (Mb), Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza na Bw. Ahmad Gamal Naibu Gavana wa Mkoa wa Alexandria wakati Mhe. Spika alipofanya ziara katika Mkoa huo tarehe 20 Juni, 2019. Wakiwa jijini Alexandria pamoja na mambo mengine, Mhe. Ndugai alikutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Alexandri na kutembelea Maktaba Kuu na Kubwa Barani Afrika (Bibliotheca Library) iliyopo Alexandria nchini Misri.