Picha ya pamoja kati ya Balozi Issa Suleiman Nassor na Uongozi wa Chuo Kikuu cha El Fayoum baada ya mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano katika sekta ya elimu na mafunzo kati ya Tanzania na Chuo hicho. Mazungumzo hayo yalifanyika tarehe 15 Novemba, 2018 kufuatia mwaliko aliopewa kutoka katika Chuo hicho. Tukio hilo lilimshirikisha Gavana wa Jimbo la El Fayoum Bw. Essam Saad Ibrahim Ahmed.
