Mhe. Balozi Issa Suleiman Nassor akikabidhiwa zawadi baada ya mazungumzo na Uongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara ya Alexandria (Alexandria Businessmen Association) tarehe 16 Oktoba, 2018. Mazungumzo ya pande hizo mbili yalisisitiza umuhimu wa kukuza na kuimarisha biashara na uwekezaji nchini Tanzania ikiwa ni sehemu ya mkakati wa utekelezaji wa sera ya Mambo ya Nje inayosisitiza juu ya diplomasia ya Uchumi.