Mhe. Balozi Issa Suleiman Nassor akipokea zawadi baada ya Mkutano wake na Jumuiya ya Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Jimbo la Behera nchini Misri tarehe 17 Oktoba, 2018. Mhe. Balozi Nassor akifuatana na Maafisa wa Ubalozi pamoja na Ofisi Mwandamizi wa Uwekezaji kutoka kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. Brendan Maro. Mhe. Balozi Nassor aliwaomba Wafanyabiashara hao na mji wa Behera kufanya ziara nchini Tanzania kwa ajili ya kuangalia fursa za Uwekezaji na Biashara.
