Mhe. Dr. Emmanuel Nchimbi mara tu baada ya kuwasili nchini Misri, akiwa na Maafisa wa Ubalozi nyumbani kwake.
Kikao cha pamoja kati ya Mhe. Dr Emmanuel Nchimbi na Maafisa wa Ubalozi pamoja na Watumishi wenyeji.

Balozi mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri Mhe. Dr. Emmanuel John Nchimbi amewasili na kupokelewa rasmi na Maafisa wa Ubalozi jana tarehe 01 Machi, 2022 saa :00 usiku kwa majira ya Cairo.

Mhe. Balozi alifika Ubalozini na kukabidhiwa rasmi dondoo za makabidhiano ya Ofisi zilizoachwa na mtangulizi wake Mej. Jen. (Mst) Balozi Anselm Shigongo Bahati, ambaye amekamilisha mkataba wake wa kazi.

Mara baada ya kuwasili Mhe. Dr. Emmanuel Nchimbi alipata nafasi ya kutembelea ofisi mbalimbali zilizopo Ubalozini na maakazi ya baadhi ya watendaji waliopo. Aidha Mhe. Balozi alifanya mazungumzo na Maafisa pamoja na Watumishi wenyeji waliopo katika Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri.