Mheshimiwa Balozi Amin Salum Ali, Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Zanzibar baada ya kufungua kongamano la Biashara kati ya Zanzibar na Misri tarehe 09 Novemba, 2018. Kabla ya kongamano hilo Mhe. Balozi Amina alipata nafasi ya kuzungumza na ujumbe wa Wafanyabiashara hao kutoka Misri kuhusu mambo mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Kiarabu ya Misri.
Ujumbe wa Misri uliongozwa na Dk. Sherif El Gabaly, Mwenyekiti wa Kamati ya Ushirikiano Afrika katika shirikisho la wenye viwanda nchini Misri.
