Mhe, Balozi Maj Gen Bahati akifanya mazungumzo na Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya Nje wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Misri Maj Gen Rashid Abdelfatah ambapo Misri imetoa ufadhili wa masomo ya miaka miwili kwa Askari Polisi wanne kutoka Tanzania. Mazungumzo hayo yamefanyika katika jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani lililopo Nasri City mjini Cairo tarehe 25 Julai, 2021.