Mkuu wa Utawala ambaye pia ni Kaimu Balozi Ndg. Makame Iddi Makame akiambatana na Ndg. Rashid Haroun - Mwambata Siasa, Nd. Athumani Thabit – Mwambata Fedha na Bi. Nimpha E. Marunda – Mwambata Utawala, alikutana na uongozi wa Kampuni ya KORRA Energi ya Misri kwa lengo la kuimarisha mahusiano katika jitihada za utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi.
Ziara hiyo ya kikazi ilifanyika tarehe 08/08/2023 katika ofisi za Kampuni hiyo eneo la Down Town – Cairo nchini Misri.
Kwa mujibu wa Bw. Mostafa Sayed Kiongozi wa Timu ya Maendeleo ya Biashara katika kampuni ya KORRAb Energi inao uzoefu wa miaka 20 sasa nchini Misri ikitekeleza miradi mbali mbali kama Contractors, utoaji huduma katika nishati endelevu ya kijani, kufanya biashara za viwandani pamoja na usimamizi na uendeshaji wa huduma katika viwanda na biashara.
Kampuni inakwenda kufanya ziara nchini Tanzania mwezi Septemba, 2023 kutafuta fursa za utekelezaji na uwekezaji katika miradi ya Nishati ambayo ni rafiki kwa mazingira, kiuchumi na watumiaji wa huduma.
Kampuni hiyo imegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni KORRA Agri, KORRA Trade na KORRA Energi kwa pamoja tayari zimeshatekeleza mradi ipatayo 220 katika sekta mbali mbali.