Mhe. Mej. Jen. Richard Mutayoba Makanzo, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri tarehe 19/05/2024 ameitembelea Kampuni ya SITES International yenye Makao yake katika mji wa Mansouria Haram, Giza nchini Misri.

Kampuni hiyo inayojishughulisha na kazi za uhandisi ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri wa michoro ya majengo, maeneo ya kumpumzikia na ujenzi kwa kuzingatia mahitaji na mazingira ya eneo husika.

Baadhi ya miradi iliyotekelezwa na Kampuni hiyo ni pamoja na ujenzi wa El Galala City huko Sokhna, Al Azhar Park, Azhar University Cairo, American University, New Cairo, J.W. Marriot Hotel, Cairo na Kadhalika.

Kampuni hiyo inatarajia kushirikiana na Kampuni ya Rowad Engineering ya Misri katika mradi wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa kisasa wa Dodoma Stadium wenye uwezo wa kuingia watu 30,000 utakaotumika katika michezo ya AFCON 27 inayoandaliwa kwa pamoja na Tanzania, Kenya na Uganda mwaka 2027.

Kampuni inayo jumla ya wafanyakazi 320 wataalamu wa fani mbali mbali katika michoro, ubunifu, usimamizi wa miradi, usimamizi wa ubora na ujenzi.

Kampuni hii ya kimataifa imeanzishwa mwaka 1986 na Dkt. Maher Stino na Dkt. Laila El-Masry Stino.

Kampuni inayo tawi lake nchini Marekani na Misri na inatarajia kuingia katika Soko la Tanzania, Afrika Mashariki na Nchi za SADC kwa ujumla.