Rais Abdel Fattah El Sisi ametuma salamu za kumtakia kheri Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kufuatia Siku ya Muungano wa Tanzania.

Katika salaam hizo zilizowasilishwa kwa Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi siku ya tarehe 02 Mei, 2023 na Mjumbe  Maalum wa Rais El Sisi Mhe. Hossam Zaatar, Rais El Sisi ameeleza kufurahishwa na kuimarika kwa uhusiano wa Tanzania na Misri na kumtakia kheri Rais Samia Suluhu Hassan katika kazi nzuri anayofanya ya kujenga Taifa la Tanzania.

Kwa upande wake Balozi Emmanuel Nchimbi alimshukuru Rais El Sisi kwa niaba ya Rais Samia S.  Hassan na kumhakikishia kuwa Tanzania inatoa kipaumbele cha pekee katika uhusiano wake na Misri.