Mhe. Meja Jenerali Anselm Shigongo Bahati Balozi wa Tanzania nchini Misri awasilisha nakala za Hati za Utambulisho kwa Mhe. Hamdi Loza, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri anayeshughulikia masuala ya Afrika tarehe 26 Desemba, 2019. Baada ya uwasilishaji huo, Mhe. Balozi Bahati na Mhe. Hamdi Loza wamezungumzia maendeleo ya ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Misri na kuazimia kuendelea kuuimarisha.

  • Balozi Bahati na Mhe. Hamdi Loza wakiwa kwenye mazungumzo ya pande mbiliBalozi Bahati na Mhe. Hamdi Loza wakiwa kwenye mazungumzo ya pande mbili