Balozi Meja Jenerali Anselm Shigongo Bahati akipata maelezo ya kiutendaji ya kiwanda cha Kampuni ya gesi ya Supreme ya Misri tarehe 02 Januari, 2020. Balozi Meja Jenerali Bahati ametembelea kiwanda hicho na kujionea uwezo wa uzalishaji na kitaalam na kuendelea kushawishi uongozi wa Kampuni kuwekeza nchini Tanzania.