Leo tarehe 31 Machi, 2022 Mhe. Dr Emmanuel John Nchimbi Balozi wa Tanzania nchini Misri amewasilisha  Hati za Utambulisho kwa Mhe. Abdel Fattah El Sisi Rais Misri. 

Wakati huo huo, Mhe. Rais wa Misri El Sisi aliwatakia Mabalozi waliowasilisha hati  mafanikio mema katika majukumu yao wakiwa nchini Misri akisisitiza kuwa Misri ipo tayari kudumisha na kulinda mahusiano mazuri yaliyopo kati yake na  Mataifa hayo katika sekta zote na kuendeleza mshikamano wake katika nyanja za kitaifa na Kimataifa.