Mhe. Meja Jenerali Anselm Shigongo Bahati, Balozi wa Tanzania nchini Misri, tarehe 19 Desemba, 2019 alifanya mazungumzo na Dkt. Muharram Helal, Mwenyekiti wa Kampuni ya 'Supreme Holding' ya Misri inayojishughulisha na uchakataji wa gesi asilia akiwa na Dkt. Mohy Hafez, Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya 'Pioneer Pharma (PPI)' ya Misri. Viongozi wa Makampuni hayo walionesha nia ya kutembelea Tanzania na kuwekeza katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.