Timu ya Taifa ya Mpira wa Wavu (Volley Ball) inayoshiriki mashindano ya Mataifa ya Afrika imefanikiwa kuingia nafasi ya 16 bora ambapo asubuhi ya leo tarehe 12 Septemba, 2023 watakamilisha ratiba kwa kugombania nafasi 13 au 14 miongoni mwa timu 16 bora.


Kocha wa Timu hiyo ameeleza kuwa hatua hiyo ni mafanikio makubwa kwa timu hiyo. Wanamichezo hao walifika Ubalozini kutoa shukurani zao kwa Serikali chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwezeshaji wake mkubwa uliowezesha Timu hiyo kushiriki vyema mashindano hayo makubwa na kuitangaza vyema Tanzania katika mchezo wa wavu. 


Shukurani nyengine zimetolewa kwa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo, Baraza la Michezo na Shirikisho la Mchezo wa Wavu. Sambamba na hayo, Ubalozi umepongezwa kwa kuiwakilisha vyema timu hiyo katika vikao vya maandalizi pamoja na mapokezi. 
Timu inatarajia kuondoka Cairo tarehe 14 usiku kurejea Tanzania baada ya kukamilisha vizuri mashindano hayo.