Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri chini ya Usimamizi wa Mhe. Balozi, Mej. Jen. Richard M. Makanzo, uliandaa hafla ya futari ya pamoja kwa Watanzania wanaoishi nchini Misri (Diaspora.)


Katika hafla hiyo, Mshauri Mkuu wa Diaspora, Bw. Seif Kibwana, alipata fursa ya kutoa nasaha zake kwa hadhira hiyo, akisisitiza umuhimu wa mshikamano, ushirikiano na kuendelea kudumisha maadili mema wakiwa ughaibuni.


Aidha, Mhe. Balozi alipata nafasi ya kuzungumza na hadhira na kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali yenye tija kwa Taifa na wananchi wake. Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni pamoja na:


• Kuimarika kwa mahusiano ya kidiplomasia na kiuchumi kati ya Misri na Tanzania.
• Ufuatiliaji na upatikanaji wa nafasi za masomo kwa Watanzania nchini Misri.
• Kusikiliza changamoto zinazowakabili wanafunzi pamoja wanadiaspora na kuangalia njia sahihi za kuzitatua kwa kuzingatia Sheria za nchi.
• Kuwasisitiza Watanzania kuishi kihalali na kuepuka vitendo vinavyokiuka sheria na maadili ya nchi wanayoishi.
• Kutafuta na kutumia fursa za uwekezaji zilizopo nchini Misri, pamoja na kuwahamasisha wawekezaji kuwekeza nchini Tanzania kwa manufaa binafsi na ya Taifa kwa ujumla.
• kukua kwa uchumi wa Tanzania ukilinganisha na miaka iliyopita.


Mwisho, Mheshimiwa Balozi aliwatakia wanadiaspora wote mfungo mwema wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, sambamba na funga ya Kwaresma huku akiwahimiza kuendeleza mshikamano, amani na upendo.